Katibu mkuu wa chama cha Riadha Tanzania (RT) Wilhelm Kidabuday amesema kitendo cha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kukubali maombi ya mwanariadha Alphonce Felix Simbu ni mapinduzi mapya.
''Ruhusa iliyotolewa na serikali imekuwa na neema na ni mapinduzi mapya waziri ameonyesha, kwamba sasa hakuna aliyemdogo wala mkubwa wote wanasikilizwa kwa maslahi mapana na taifa'', amesema Gidabuday leo kwenye mahojiano na East Africa Television.
Hivi karibuni mwanariadha Alphonce Felix Simbu aliwasilisha maombi kwa chama hicho akiomba kuondolewa kwenye orodha ya wanariadha wa Tanzania watakaoshiriki mbio za Jumuiya ya Madola huko Australia ili ajiandae na mbio za riadha za London, na chama hicho kiliwasilisha maombi hayo kwa wizara husika, ambapo jana Wizara ilitoa baraka zote kwa Simbu.
Aidha Buday amesema wao kama Chama cha Riadha wameamua kuwa na utaratibu wa kuwasikiliza wanariadha wao wanataka nini, kwasababu wao ndio wenye uwezo wa kukimbia na kuleta medali ndio maana wamelifanyia kazi ombi la Simbu.
Kwa upande wa wanariadha wengine ambao wanaendelea na maandalizi ya kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya Jumuiya ya Madola na mbio za Riadha za Dunia zitakazofanyika Valencia Hispania wamesema wamefurahishwa na uamzi wa Simbu kwani unatoa nafasi ya wao kushiriki na kuwakilisha taifa.

No comments:
Post a Comment