Ronaldo de Assis Moreia mzaliwa wa Mji wa Porto Alegre nchini Brazil akiwa na miaka 37 ametangaza kustaafu soka la ushindani baada ya kcheza kwa takribani miaka 20.
Kaka wa nyota huyo wa zamani wa Brazil na vilabu vya PSG, Barcelona na AC Milan ambaye pia ni wakala wake Roberto de Assis usiku wa kuamkia leo ameweka wazi kuwa mdogo wake huyo ameachana rasmi na soka la ushindani.
Matukio ya kukumbukwa kutoka kwa Ronaldinho.
Kombe la dunia 2002 Brazil vs England
Ronaldinho akiwa na miaka 22 aliishangaza dunia baada ya kufunga bao kupitia mpira wa adhabu ndogo mita 35 kutoka golini, wakati nchi yake ilipokuwa imefungana bao 1-1 na England hivyo kufunga bao la pili kwa mkwaju wa kushangaza lakini baadaye alitolewa kwa kadi nyekundu. Brazil ilitwaa ubingwa wake wa tano mwaka huo.
Bao lake la Stamford Bridge 2005
Ronaldinho pia anakumbukwa kwa kufunga bao la aina yake kwenye uwanjwa wa nyumbani wa Chelsea Stamford Bridge ambapo akiwa na Barcelona kwenye mchezo wa Ligi ya mabingwa barani Ulaya. Ronaldinho alipokea pasi kutoka kwa Iniesta kisha akawazubaisha mabeki Jonh Terry na Ricardo Carvalho kwa kuchezesha mguu na kiuno chake na baadae kupiga shuti lililozaa goli.
Kupigiwa makofi na mashabiki wa Real Madrid 2005.
Novemba 2005, Ronaldinho alipata heshima ya kupigiwa makofi kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu baada ya kuisaidia Barcelona kushinda 3-0 huku yeye akifunga mabao mawili na kuonyesha kiwango cha hali ya juu.
Bao lake la 33 na la mwisho Brazil
Ronaldinho alicheza mechi yake ya mwsiho na timu ya taifa ya Brazil mwaka 2011. Mechi hiyo ilikuwa ya kirafiki dhidi ya Mexico ambapo alipewa nafasi ya kuwa nahodha. Katika mechi hiyo alifunga bao lake la 33 na la mwisho kwa timu ya taifa kupitia mkwaju wa adhabu ndogo kutoka mita 35.

No comments:
Post a Comment