
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe jana Januari 20, 2018 alifunga safari na kumtembelea msanii wa filamu nchini Wastara Juma Sajuki ambaye anasumbuliwa na tatizo la mguu.
Waziri Mwakyembe aliongozana na Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza na Mtendaji Mkuu Bodi ya Filamu Joyce Fissoo ambapo pamoja na kumsalimia Waziri Mwakyembe aliweza kumchangia msanii huyo kiasi cha shilingi Milioni moja ili kumsaidia kuweza kupata zaidi milioni 18 zinazohitajika kwa ajili ya matibabu ya mguu huo.
Mbali na hilo Dr. Mwakyembe ametoa wito kwa wadau wa Sanaa na Watanzania kwa ujumla kuungana katika kupata kiasi hicho cha Tsh.18 M ili kufanikisha matibabu yake na kumrejesha katika hali ya utendaji wa kazi zake za Sanaa.
Msanii Wastara Juma aliweka wazi kwa jamii juu ya tatizo lake la maumivu ya mguu ambapo inahitajika milioni 18 ili kumuwezesha kwenda kufanyiwa matibabu zaidi nchini India
No comments:
Post a Comment