Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amefunguka na kusema kuwa baadhi ya walimu ambao wamekuwa wakichukua michango ya wazazi na wanafunzi na kuzipeleka kwenye mambo yao binafsi watashughulikiwa.
Jafo amesema hayo leo akiwa Ikulu jijini Dar es Salaama alipokutana na Rais Dkt. John Pombe Magufuli na kusema amepata taarifa kuwa kuna baadhi ya walimu wamekuwa wakitumia fedha za michango katika mambo yao binafsi na kusema ni lazima wachukuliwe hatua.
"Nina taarifa ambayo naifanyia kazi kwamba kuna baadhi ya walimu fedha zile wanazipeleka katika matumizi yasiyokusudiwa kuhakikisha zinatatua matatizo yao, kuna taarifa nyingine nimepata kutoka halmshauri ya Songea kuanzia leo hii tutaanza kufanya uhakiki maeneo mbalimbali itakapo bainika ndani ya wiki hii tutaanza kuwachukulia hatua wale watu wote ambao wameshiriki katika jambo hili kwa kuwa walipewa muongozo lakini wamekiuka kwa makusudi" alisema Jafo
Waziri Jafo amesisitiza kuwa hatua kali zitaanza kuchukuliwa ndani ya wiki hii na kuwataka wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuhakikisha mpaka siku ya Ijumaa wawe wamefikisha taarifa za shule ambazo zilifanya jambo hilo na kukiuka utaratibu wa Serikali.
"Tunataka kuanza kuwachukulia hatua Wakuu wa shule, Maafisa Elimu katika halmshauri hizo kwa sababu hatuwezi kuvumilia jambo ambalo lilishatolewa muongozo na watu wanaendelea kufanya tofauti, tunataka kila mtu atimize wajibu wake kwa ajili ya kuhakikisha mwananchi mnyonge anapata huduma kama Serikali yake na Rais wetu alivyokusudia"
No comments:
Post a Comment