Pierre kuendeleza ubora wa Djuma Simba ? - HD NEWS

Breaking

Habari za Uhakika

Socialize

Wednesday

Pierre kuendeleza ubora wa Djuma Simba ?


Image result for Pierre Lechantre
Klabu ya soka ya Simba imethibitisha kuwa kocha wake mkuu mpya Pierre Lechantre, leo ameanza kazi rasmi ya kukinoa kikosi hicho ambacho kipo kwenye ubora kikiwa kinaongoza msimamo wa ligi.


Kocha huyo raia wa Ufaransa kwa kushirikiana na kocha wa viungo raia wa Morocco Aymen Mohammed Habib wanaanza kazi wakiwa na kibarua cha kuendeleza ubora ulioonyeshwa na kocha msaidizi wa timu hiyo Masoud Djuma.

Kocha huyo ambaye wiki iliyopita alisaini mkataba na Simba ambao haujawekwa wazi kuwa ni wa muda gani, atakuwa na jukumu la kuitengeneza Simba SC kuwa na uwezo wa kushindana kimataifa hususani kwenye michuano ya kombe la shirikisho Afrika.



Kocha msaidizi Djuma amekuwa na mwendelezo mzuri katika ligi kuu tangu aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Joseph Omog afukuzwe kazi baada ya kupoteza mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya Green Worriors.

Msimu huu Simba imepoteza mchezo mmoja tu ambapo hadi sasa kwenye ligi haijapoteza mechi zake 14 ilizocheza ikifanikiwa kuvuna alama 32 na kujikita kileleni. Kazi inabaki kwa kocha huyo wa zamani wa Cameroon kuendeleza alipofikia Masoud Djuma.

No comments:

Post a Comment