Ndege hiyo isio na rubani yenye nafasi ya watu wawili iliruka kwa dakika tano katika pwani ya ghuba.
Ndege hiyo ilitazamwa ikipaa angani na mwanamfalme Hamdan bin Mohammed.
Dubai ina malengo makubwa ya kuwa mji wa kiteknolojia huku ndege zisizo na rubani na roboti zikihusika pakubwa katika mpango huo.
Ndege zisizo na marubani kubeba abiria
Abiria kubebwa kwa ndege zisizo na marubani Dubai
Ndege zagongana nchini Canada
Ndege yaangukia nyumba,watu wote wanusurika Marekani
Ndege hiyo ya teksi ilibuniwa na kampuni ya Ujerumani ya Volocopter na kampuni hiyo imesema inatumai kwamba ndege hiyo itaanza kufanya kazi katika kipindi cha miaka mitano.
''Utumizi wake utahusisha simu aina ya smartophone, programu na kuagiza ndege hiyo kuruka hadi katika eneo unalopania kuelekea'', alisema Afisa mtendaji wa kampuni hiyo Florian Reuter
Teksi ndege isiokuwa na rubani awali ilifanyiwa majaribio nchini Ujerumani mnamo mwezi Aprili.
Kampuni pinzani ya China eHand ilitarajiwa kuwa ya kwanza kuzindua msafara wa teksi ndege mjini humo lakini mipango yake ikaonekana kuchelewa.
Dubai imejiweka kuwa mji wa kiteknolojia duniani ikiwa na mipango ya magari ya kujiendesha kusimamia robo ya safari zote kufikia 2030.
Noel Sharkey ambaye ni mwanasayansi wa komyuta na ambaye pia ni mtaalam wa roboti katika chuo kikuu cha Sheffield alisema kuwa: Changamoo kuu itakuwa vikwazo visivyoepukika kama vile kukwepa teksi nyengine, majumba marefu, vindege na ndege zisizokuwa na rubani ambazo zinatumika kusafirisha mizigo.

No comments:
Post a Comment