Korea Kaskazini yadai Marekani imetangaza vita - HD NEWS

Breaking

Habari za Uhakika

Socialize

Tuesday

Korea Kaskazini yadai Marekani imetangaza vita



Waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini amedai kwamba rais wa Marekani Donald Trump ametangaza vita dhidi ya taifa hilo.
Ri Yong-ho aliwaambia waandishi wa habari kuwa Korea Kaskazini ina haki ya kudungua ndege za vita za Marekani.
Hi ni hata kwa zile ndege zenye hazipo katika anga ya Korea Kaskazini, aliongeza waziri huyo.
Pande hizo mbili zimekuwa zikitupiana maneno makali.
Licha ya majuma kadhaa ya misukusuko, wataalamu wanasema kuwa hakuna uwezekano wa makabiliano ya moja kwa moja kati ya Marekani na Korea Kaskazini.
Korea Kaskazini: Hotuba ya Trump ni sawa na mbwa anayebweka
Viongozi wa Marekani na Korea Kaskazini watupiana vitisho vipya
Baada ya Bw Ri kuhutubia Umoja wa Mataifa siku ya Jumamosi, Rais Trump alijibu kupitia mtandao wa twitter, akisema kuwa Bw. Ri na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un hawatakuwepo kwa muda ikiwa wataendelea na maneno yao.
Jibu la Bwana Ri lilikuja wakati akiondoka New York baada mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa.

Korea Kaskazini imeendelea na majaribioya makombora ya nyuklia na ya masafa marefu siku za hivi karibuni licha ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa.
Viongozi wa nchi hiyo wanasema kuwa uwezo wake wa zana za nyulia ndiyo njia pekee dhidi ya mataifa yanayotishia kuiharibu.

Trump na Kim Jong-Un waitana ''wenda wazimu''
Baada ya jaribio la hivi majuzi na kubwa zaidi la nyulia mapema mwiezi huu, baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, liliidhinisha vikwazo vipya dhidi ya nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment